Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative ifikapo Juni 7, na kutoa muda wa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Akizungumza leo Mei 24, huko Downing Street, Theresa amesema amefanya kila lililokuwa ndani ya uwezo wake ili aweze kutekeleza matokeo ya kura za maoni kuhusu Umoja wa Ulaya (EU) ya mwaka 2016.
“Nimefanya kila niwezalo ili kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mwaka 2016, ni jambo lilibakia kuwa na majuto mengi kwamba nimeshindwa kutimiza Brexit – Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya lakini Waziri Mkuu mpya ndio suluhisho,” amesema Theresa.