24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

TFS yakabidhi madawati 120 shule ya msingi Kipera wilayani Mvomero

Na Mwandishi Wetu, Mvomero

WANANCHI wa Kijiji cha Kipera katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wametoa pongezi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) baada ya Wakala huo kukabidhi madawati 120 yenye thamani ya Sh.Milioni 12.6 kwa shule ya Msingi Kipera.

TFS mbali ya kukabidhi madawati hayo leo Oktoba 18,21 ,pia meahidi kuwa atamalizia madawati 70 ambayo yamebakia ili kukamilisha idadi ya madawati 190 yanayohitajika kwa shule ya Msingi Kipela yenye jumla ya wanafunzi 1,110.

Akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa kwa madawati hayo mbele ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, walimu, wazazi, wananchi pamoja na wanafunzi Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo amesema Wakala huo unaowajibu wa kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto ndani ya jamii.

“Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) pamoja na shughuli zetu za usimamizi wa misitu na rasilimali zitokanazo na misitu ,tumekuwa tukishiriki katika kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali, hiki ambacho tumekifanya kwa Shule ya Msingi Kipera tumekuwa tukikifanya na katika maeneo mengine.

“Leo tumekabidhi madawati 120 lakini katika taarifa ya Mwalimu Mkuu wa Shule amesema wakipata madawati mengine 70 watakuwa wamemaliza changamoto ya uhaba wa madawati.Hivyo niwaahidi tutaleta madawati hayo 70 ili wanafunzi wetu wasome katika mazingira mazuri.

“Pia tutamalizia ujenzi wa madarasa mawili ambao ujenzi wake tumeambiwa haujakamilika, tunafanya haya kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Samia ambaye amedhamiria kuboresha sekta ya elimu nchini ,”amesema Profesa Silayo huku akiwapongeza walimu, wazazi na wanafunzi kutokana na mafanikio ambayo shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1976 imeyapata ikiwemo ufauli mzuri wa wanafunzi ambao wamekuwa wakiupata mwaka hadi mwaka.

Akifafanua zaidi mbele ya wananchi wa Kijiji hicho kwamba Wakala huo ni wa Serikali na umepewa jukumu la kusimamia rasilimali za misitu na nyuki,hivyo ni wajibu wao kuhakikisha nyuki wanakuwepo.”Tunasimamia pia misitu, na hata mkiona miti ni kazi yetu, tunasimamia misitu nchi mzima.

“Tunapata mvua kwasababu ya uwepo wa misitu, wanyama wanaishi msituni. Ukiwa na miti unapata mazao ya aina mbalimbali na yote hayo yanatokana na kutunza na kuhifadhi misitu.Matunda mazuri yayofanywa na TFS tumeona  wanafunzi wa kipera nao wanayafaidi.”

Profesa Silayo amesisitiza Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri ya kuwatumikia Watanzania, hivyo wao wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kukabidhi madawati hayo na kumalizia yaliyobakia pamoja kuboresha miundombinu ya madarasa mawili.

“Tutashirikiana kuboresha mazingira mazuri ya shule ya msingi Kipela, Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Naibu Waziri walipanga kuwepo lakini katika tukio hili lakini kutokana na kuwa na majukumu mengine nimewawakilisha,hata hivyo wamenituma nije niwaambie tuendelee kutunza rasilimali za misitu ,miti ,ikolojia na nyuki,”amesisitiza na kuongeza Rais Samia  amesema kazi iendelee hivyo TFS wataendelea kuwatumikia wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye ndio Ofisa Elimu Msingi katika wilaya hiyo Maajabu Nkanyemka ameshukuru kupatikana kwa madawati hayo ,amewaomba walimu,wanafunzi na wazazi kushirikiana kuyatunza.

“Tunahidi madawati haya tutayatunza, tutayatumia vizuri kama ilivyokusudiwa, tunaka kuona yanatumika kwa wanafunzi waliopo na wanaokuja.Kwa kuwa TFS lwameahidi madawati mengine 70 basi suala la matengenezo ya madawati watakayoharibika tutafanya halmashauri ya Mvomero.

“Yanayofanywa na Rais Samia  katika elimu ,ni wajibu wetu sisi halmashauri kuunga mkono juhudi zake kwa vitendo, na hiki ambacho kimefanywa na TFS  ni sehemu ya kuonesha kuunga mkono kazi inayofanywa na Rais,”amesisitiza.

Awali akizungumza kwa niaba ya walimu,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kipera William Rufili amesema wanashukuru changamoto ya uhaba wa madawati kupata ufumbuzi wake pamoja na majengo mawili ya madarasa, lakini pia ametoa ombi kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia kwani wanayo changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo.

“Jumuiya ya Kipera na kata ya Mlali wamefurahia ugeni wa TFS kutokana na lengo ambalo limetukutanisha , shule yetu imepitia hatua mbalimbali za maendeleo , na kwa sasa inajumla wanafunzi 1,110 na walimu 24 .Taarifa ya miundombinu, jumla ya vyumba vya madarasa vinavyohitajika ni  25 lakini kwa sasa vipo 11 na viwili havijapakamilika 

“Jitihada za wananchi wamefikia hapo hivyo bado tunahitaji msaada wa wananchi na Serikali katika madawati , tunao upungufu wa madawati 190 baada ya kukabidhiwa leo madawati 120 yamebakia madawati 70,hivyo tunawaomva TFS mtusaidie,”amesema.

Mwanafunzi Moshi Salum anayesoma darasa la sita katika shule hiyo ametoa pongezi kwa TFS kwa msaada huo wa madawati lakini akatoa ombi iwapo itawezekana kwa TFS iwasaidie katika kuwajengea ofisi za walimu,viti pamoja na meza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles