28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu: Michezo itumike kuboresha afya na ufanisi kazini

Na Zuena Msuya, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ameiasa Timu ya Wanamichezo wa Wizara ya Nishati inayoshiriki Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), kutumia Michezo hiyo kama sehemu ya kuboresha Afya na ufanisi sehemu za kazi.

Mhandisi Masanja amesema hayo mkoani Dodoma wakati akitoa nasaha kwa wachezaji hao wanaokwenda kushiriki SHIMIWI mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba 2, 2021.

Aidha amewataka wanamichezo hao kuheshimu Michezo hiyo na kuzingatia dhana nzima ya kuanzishwa kwake.

Vilevile aliwasihi wanamichezo hao kucheza kwa nidhamu pamoja na kuwa na mbinu za ziada ili kupata ushindi wa kishindo.

Sambasamba na hilo amewaeleza kuwa wanapokuwa kambini wanapaswa kuishi kwa nidhamu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara hiyo Ziana Mlawa aliwaeleza wanamichezo hao kuwa wanapokuwa kambini ni sawa na wanapokuwa maeneo yao ya kazi hivyo wafuate na kuzingatia taratibu zote za kiutumishi.

Mlawa alisema kuwa wanamichezo hao wakawe mfano bora kiutendaji kwa kushiriki mazoezi ya aina yote na yale yote wanayopaswa kufanya wanapokuwa katika michezo hiyo.

Vilevile aliwasihi kuendeleza umoja, ushirikiano kwa wanamichezo wote watakaokuwa pamoja kama wanavyoshirikiana na watumishi wengine katika wizara ya Nishati.

Takribani wanachezo 30 kutoka Vitengo na Idara za wizara hiyo watashiriki michezo ya Mpira wa Pete, Miguu, kuvuta kamba, kuendesha Baiskeli, mbio za Magunia nk.

Michezo ya SHIMIWI inatajiwa kufunguliwa Octoba 20, 2021 na kufikia kilele chake Novemba 2, 2021 mkoani Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles