Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewaadhibu wachezaji Bernard Morrison wa Simba na Mukoko Tonombe wa Yanga kwa makosa waliyofanya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Azam Sports Federation Cup(ASFC) ulikutanisha timu zao Julai 25, 2021 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Kwa Mujibu taarifa ya TFF, Morrison amepigwa faini ya sh 3,000,000 na kufungiwa mechi tatu kutokana na kosa la kimaadili, nidhamu na udhalilishaji kinyume na kanuni.
Mukoko ametozwa faini ya sh 500,000 na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la la kumpiga John Bocco.
Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Mohammed Nabil, amepigwa faini y ash 500,000 kwa kugoma kuhudhuria mkutano wa maandalizi ya mcheza na waandishi wa Habari.
Katika hatua nyingine Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh 4 milioni kwa makosa matatu tofauti, huku viongozi wakipewa onyo kutokana na kukaidi maelekezo na kuingilia utaratibu uliowekwa katika shughuli ya kugawa medali kwa washindi.
Kwa upande wa klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh 4.5 kwa makosa matano tofauti ikiwamo viongozi wake kuingia uwanjani wakitumia mlango usio rasmi na kuambatana na watu wasiokuwa na tiketi.