Hassan Daudi na MItandao
Mshambuliaji wa Kibrazil, Neymar, ameweka wazi kuwa kuna mazungumzo ya mkataba mpya kati yake na PSG.
Neymar (29), amedai kuwa kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo haitashangaza kubaki PSG baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwakani.
CHANZO: RMC Sport
Stone akaribia mkataba mpya
Beki wa kati wa Manchester City, John Stones, atasaini mkataba wa kumbakiza klabuni hapo hivi karibuni.
Mwaka jana, Stone aliyetua Man City mwaka 2016 akitokea Everton alikuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Etihad.
Mkataba huo wa miaka mitano unatajwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 39 na Stone atakuwa akiingiza Pauni 150,000 (zaidi ya Sh mil. 180 za Tanzania).
Liver wamtenge dau Konate
BADO Liverpool wanaifukuzia saini ya beki wa RB Leipzig, Ibrahima Konate.
Ili kukamilisha dili hilo, Liverpool wametenga kitita cha Pauni milioni 40 (zaidi ya Sh bil. 120 za Tanzania). CHANZO: Mail
Barca wamuibukia De Ligt
Klabu ya Barcelona imeonesha nia ya kumsajili beki wa Juventus na timu ya taifa ya Uholanzi, Matthijs de Ligt.
De Ligt mwenye umri wa miaka 21, aliwahi kutakiwa Barca akiwa Ajax lakini Juve walijiongeza na kuinasa saini yake. CHANZO: Sport
Rodgers: Sitaki kazi Tottenham
KOCHA wa Leicester City, Brendan Rodgers, havutiwi na kibarua cha kwenda kuinoa Tottenham iliyomtimua Jose Mourinho.
Na badala yake, Rodgers anatamani kuendelea kuitumikia Leicester aliyoifanya kuwa timu tishio Ligi Kuu ya England. CHANZO: Sky Sports
Flick aitwa mezani Ujerumani
Chama cha Soka cha Ujerumani kimeanza mazungumzo na kocha atakayeondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu, Hansi Flick.
Hayo yanaibuka huku ikifahamika kuwa hata Jurgen Klopp wa Liverpool naye anahusishwa na kibarua hicho kinachoshikiliwa na Joachim Low. CHANZO: 90min