23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Madrid 1-1 Chelsea Rekodi muhimu

Madrid, Hispania

Thomas Tuchel hajawahi kufungwa na Real Madrid katika mechi zote tano alizokutana nayo Ligi ya Mabingwa. Mjerumani huyo ameshinda moja na kutoa sare nne.

Chelsea haijashinda hata mechi moja ya nusu fainali kati ya nane ilizocheza ugenini. Katika mechi hizo, imefungwa tatu na kutoa sare tano.

Real Madrid ilipiga shuti moja tu lililolenga lango dhidi ya Chelsea.

Bao dhidi ya Chelsea lilikuwa la 71 kwa Karim Benzema tangu aanze kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Christian Pulisic amekuwa mwanasoka wa kwanza raia wa Marekani kupachika bao katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pulisic amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuifungia Chelsea katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Amefunga akiwa na miaka 22 na siku 221).

Beki wa Chelsea, Thiago Silva, amekuwa mchezaji ‘mzee’ zaidi kuingia kikosi cha kwanza cha Chelsea kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Ana miaka 36 na siku 217).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles