Kigali, Rwanda
Watu nchini Rwanda wameyakimbia makazi yao kufuatiwa tetemeko la ardhi lililotekea siku ya Jumanne Mei 26, 2021 katika mji wa Gisenyi Magharibi mwa Rwanda.
Tetemeko hilo lililosababishwa na mlipuko wa Volkano uliotokea nchi jiraniya Jamuhuri ya Kimedemokrasia ya Congo DRC siku ya Jumamosi Mei 22, 2021.
Wataalamu wa kufuatilia matetemeko ya ardhi nchini Rwanda kimeripoti matetemeko ya ardhi yaliyofikia kiwango cha 5.3 na 5.1 katika vipimo vya richa Jumanne na Jumatano asubuhi.
Mamlaka nchini Rwanda imetoa wito wa utulivu na kusema kuwa imechukua hatua ya kuwasaidia watu walio katika hali ya hatari, baada ya nyumba kadhaa kuharibiwa.
Shule, benki, soko na maduka yamefungwa, huku watu wakilala nje usiku wa Jumanne kwa kuhofia nyumba zao kuporomoka na kuwaangukia.
Pia baadhi ya watu walionekana Jumatano asubuhi katika kituo kikuu cha usafiri wakijaribu kuondoka Gisenyi kuelekea maeneo ya mashariki.
Hospitali katika mji huo zilihamisha baadhi ya huduma na wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika maeneo ya magharibi na kaskazini mwa Rwanda.