26.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 15, 2021

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzungumza na Mali

Bamako, Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura siku ya Jumatano kujadili hali nchini Mali, baada ya jeshi kuchukua tena uongozi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kanali Assimi Goita ambaye pia ni Makamu wa rais alitoa armi ya kukamatwa kwa rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu  Moctar Ouane na kufuta serikali ya mpito baada ya kuwashtumu viongozi hao wawili kwa kutomshirikisha kuhusu mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Hayo yanajiri wakati mpatanishi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, Goodluck Jonathan, aliwasili jana, Jumanne Mei 25 alasiri, huko Bamako kujaribu kuzuia mgogoro uliosababishwa na mapinduzi mapya yaliyoendeswa na kuli la wanajeshi waliohusika na mapinduzi ya mwezi Agosti 2020.

Mazungumzo yalioanza jana jioni, huko Bamako, kati ya Goodluck Jonathan na ujumbe wake upande mmoja, na kwa upande mwingine na wawakilishi wa viongozi wa mapinduzi ya zamani.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,753FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles