31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Teni The Entertainer aachia ‘Wondaland’

Lagos, Nigeria

Mwandishi staa nchini Nigeria, Teni The Entertainer , ameachia albamu yake mpya ‘Wondaland’, ambayo ilianza kupatikana sokoni, Machi 19, mwaka huu.

Albamu hiyo imefungua mafanikio mapya kwa staa huyo ulimwenguni, ambapo miongoni mwa singo zinazofanya vizuri zaidi kwa sasa ni ‘For You’ aliyopiga kolabo na msanii ‘hot cake’ nchini humo, Davido.

Video ‘For You, imetazamwa na watu milioni 14 kwa sasa huku ukishikilia namba moja kwenye chati za Apple Music Nigeria.

Aidha, wimbo huo upo kwenye 10 Bora za nyimbo bora za Afrobeats zinazochezwa nchini Uingereza, huku ikiwa kwenye 20 Bora kwenye nyimbo zinazosikilizwa ulimwenguni kote.

Baada ya Teni kufanya kazi kwa miaka miwili katika miji saba kote ulimwenguni ikiwemo, London (Uingereza), New York (Marekani), Dubai (Falme za Kiarabu), Orlando (Marekani), Ondo (Nigeria), Lagos na Abuja (Nigeria).

Teni aliona albamu hiyo kama kazi ya upendo na kitu ambacho kitampa shabiki burudani ya aina yake kuanzia wimbo wa kwanza hadi wa mwisho.

Teni anasema: “Nilitaka kutoa albamu ambayo kila mmoja kutoka katika mji wa ardhi ya mama yangu, Ondo au mji wa baba yangu – Ekiti mpaka Osaka, Japan wanapata burudani ya aina yake, lakini pia elimu kupitia albamu hiyo.

“Nina imani albamu hii inaweza kuishi na kusikilizwa hata kwa miaka zaidi ya 20 ijayo, kutokana na ujazo na ubora uliomo ndani yake.”

Staa huyo anamiliki tuzo kadhaa za muziki zikiwemo za Mwimbaji Bora, Mwandishi Mashahiri Bora, Mtumbuizaji Bora na nyingine nyingi nchini humo.

Anamalizia kwa kusema: “Ni albamu ambayo haichoshi kuisikiliza. Siyo kwamba ni nzuri kwa sababu inatoka kwa msanii wa Kiafrika, bali kwa sababu ni muziki safi na zawadi ya pekee kutoka ndani kabisa ya moyo wangu.
“Nimekuwa nikiifanyia kazi hii albamu kwa miaka miwili katika miji saba ulimwenguni – London, New York, Orlando, Dubai, Ondo, Lagos na Abuja. Lengo ni kupata mchanyato mzuri ambao utakonga nyoyo za wasikilizaji wangu na ndicho nilichokifanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles