28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

“Acheni kuua wafanyabiashara”-Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, kutanua wigo wa ukusanyaji kodi huku akionya tabia ya kuwaua walipa kodi kwa kufunga biashara zao, kuchukua fedha na vifaa vyao vya kazi pamoja na kufunga akaunti zao.

Rais Samia amesema hayo leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, akibainisha kuwa vitendo hivyo vinasababisha wafanyabiashara kuhamia nchi jirani.

Aidha, amesisitiza agizo lililotolewa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliyeagiza makusanyo ya Serikali kwa mwezi kuanza kuwa Sh trilioni 2.

“Kama alivyosema Makamu wa Rais hapa, nendeni mkatanue wigo wa kodi na mtengeneze walipa kodi wengi zaidi. Trend mnayoenda nayo ni kuua walipa kodi, wafanyabiashara. Mnatumia nguvu kubwa kuwakamua, mnachukua vifaa vyao vya kazi mnakwenda kufungia akaunti zao mnachukua fedha kwa nguvu kwenye akaunti zao.

“Matokeo yake, akitoka hapo anakwenda kufunga biashara anahamia nchi jirani naombeni sana nendeni mkaongeze walipa kodi yale yanayopunguza walipa kodi mkayasimamie. Tunamaliza Pasaka Jumatatu pengine Jumanne tukaja hapa kuapishana na wengine,” amesema Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles