26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tenga apewa ubalozi wa heshima TFF

tengaNA GRACE HOKA, TANGA

RAIS mstaafu wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Leodegar Tenga, ameteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutokana na kuwa kiongozi mzuri wakati akiwa madarakani.

Uteuzi huo umekuja baada ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kutoa mapendekezo kwa wajumbe waliokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo uliofanyika katika Hoteli ya Naivera mjini Tanga, kisha wajumbe kupitisha jina lake.

Wajumbe walipitisha jina hilo kutokana na kufanya kazi vizuri wakati akiwa Rais wa TFF kwa vipindi viwili tofauti.

Akisoma wasifu wa Tenga, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo, alisema Tenga aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya soka ya Taifa miaka ya 80 akiwa nahodha  na kuiwezesha kufika hatua ya fainali nchini Nigeria.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, jana alizindua eneo la ujenzi wa uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000 katika eneo la Mnyanjani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwantumu alisema eneo hilo likijengwa na kutumiwa vizuri litaweza kuzalisha wanasoka wengi ambao baadaye wataweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

“Kama eneo hili litajengwa uwanja mzuri na ukatumiwa ipasavyo, baada ya miaka mitano ijayo naamini tutakuwa na vijana wengi kwenye timu zetu pamoja na kikosi cha timu ya Taifa ambao wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika soka.

“Naahidi nitakuwa msimamizi mkuu wa kituo hiki lakini pia naishukuru TFF kwa kupata wazo la kujenga uwanja huu katika Mkoa wa Tanga, hii ni fahari kwetu kwani walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo katika mikoa mingine,” alisema.

Kwa upande wake, Rais wa TFF, Malinzi alisema ujenzi wa uwanja huo utaenda sambamba na kituo cha kukuza na kuendeleza soka Academy na pia kutakuwa na hoteli yenye hadhi ya nyota tatu.

Malinzi alisema wanatarajia kila mkoa uwe na kituo kama hicho cha michezo kwa kuwa jambo hilo linaendana na ilani yake ya uchaguzi.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles