27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

TENDWA AJITOSA KESI YA MAUAJI NDUGU WA FAMILIA MOJA

MANENO SELANYIKA Na MAMII MSHANA (Tudarco)–Dar es Salaam

ALIYEKUWA Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amejitosa kuwatetea ndugu watatu wa kiume kutoka familia moja wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji ya dada yao.

Tendwa ambaye kwa sasa ni wakili wa kujitegemea, anawatetea watuhumiwa hao ambao ni Robert Bugaisa, Richard Bugaisa na Godfrey Bugaisa.

Watuhumiwa hao walifikishwa juzi katika Mahakama ya Kinondoni mbele ya Hakimu, Boniphace Lihamwike, Wakili wa Serikali Tumaini Mfikwa, aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa kwa sababu upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

“Mheshimiwa PI kesi namba 14/2016 watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama yako wanakabiliwa na shtaka la mauaji, lakini bado jalada la kesi hii lipo kituo cha polisi kwa uchunguzi wa tukio hilo,” alidai Wakili Tumaini.

Wakili wa utetezi, Tendwa alidai kwamba hana pingamizi dhidi ya maelezo ya upande wa mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo.

Naye Hakimu Lihamwike, alisema kwa mujibu wa sheria mahakama  hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kwamba pindi upelelezi utakapokamilika kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu.

Hivyo mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo, imedaiwa kuwa Julai 26, mwaka jana saa 4 usiku maeneo ya Boko CCM, marehemu Selina aliingiliwa na watu wasiojulikana na kuuawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles