24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BODI YA MIKOPO YAWATAKA WANAFUNZI KUZINGATIA MUDA

NA TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanafunzi wanaohitaji kuomba mkopo katika bodi hiyo kufanya hivyo ndani ya muda uliopangwa, ili kuepuka usumbufu.

Akizungumza na MTANZANIA, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa, alisema wanafunzi wengi wamekuwa wakisubiri dakika za mwisho ndipo wanaomba.

Alisema kwa kuwa maombi yote yanafanyika kwa mtandao, siku za mwisho mtandao umekuwa ukielemewa na kushindwa kufanya kazi vizuri.

“Hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa waombaji watakaoshindwa kuomba katika muda uliopangwa, hivyo nawasihi wafanye hivyo mapema kabla ya kuzimwa kwa mtambo,” alisema Dk. Mwaisobwa.

Alisema waombaji wengi pia hawasomi na kuelewa mwongozo wa utoaji wa mikopo, jambo linalosababisha kufanya makosa katika maombi yao.

“Niwaombe wazazi na wanafunzi kusoma kwa makini na kuelewa mwongozo huo wasije kufanya makosa yatakayosababisha kushindwa kupata mkopo,” alisema Dk. Mwaisobwa.

Aidha, Mwaisobwa aliongeza kuwa, HESLB imefungua dirisha la maombi ya mkopo tangu Agosti 6, mwaka huu na linatarajiwa kufungwa Septemba 4, mwaka huu.

“Baada ya hapo tutafanya uchambuzi wa wanufaika na Septemba 16, mwaka huu, tutatoa orodha ya majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo,” alisema Mwaisobwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles