26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

TEKNOLOJIA YA 5G ITAKAVYOIBADILI DUNIA 2020

 

Na MWANDISHI WETU

DUNIA inaelekea kuendeshwa na watu wenye akili, ambao wanatumia teknolojia au digitali kufanya kila jambo kuwa rahisi kupitia huduma nyingi kuanza kutolewa kwa mfumo wa intaneti.

Ni wazi kuwa teknolojia tunakoelekea itakuwa inahusika kwenye kila kitu kwa sehemu kubwa zaidi na hapo ndipo tutakaposhuhudia ipi ni teknolojia ya kweli kwani ushindani unazidi kuongezeka kila kukicha.

Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyowekwa wazi na wanateknolojia yatakayoenda sambamba na kasi ya 5G.

 

Uwezo bandia kuchukua nafasi

Tarajia kushuhudia akili za bandia zikichukua nafasi kubwa zaidi pindi kasi hii ya intaneti ya 5G itakapoanza kutumika, tunaambiwa kuwa uwezo huu wa Artificial Intelligence (AI) utaongeza ufanisi zaidi wa kazi na huduma bora zaidi ikilinganishwa na uwezo wa binadamu.

Hivyo, ni wazi kuwa kuanzia 2020 dunia inatarajia mapinduzi makubwa zaidi ya teknolojia kupitia ujio wa intaneti ya 5G ambapo kutakuwa na programu (Apps) na vifaa maalumu vitakavyotumika kusukuma teknolojia hii bila kusahau eneo la taarifa (data).

Maeneo kama benki na ofisi mbalimbali duniani zinaelezwa kuanza kuendeshwa zaidi na uwezo wa teknolojia tofauti na binadamu kama inavyotumika hivi sasa, ambapo huduma zitatolewa haraka na kwa ufanisi wa kiwango cha juu tofauti na sasa.

Pia wameenda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa kutakuwa na ‘application’ ambazo zitakuwa zikitumia teknolojia kama Virtual Personal Assistants (VPAs), kwa ajili ya kufanya kazi zote zinazofanywa kwenye ofisi mbalimbali kila siku, ikijumuhisha kuandika na kutuma barua pepe.

Tambua kuwa ‘application’ hizi pia zitaruhusu kupokea teknolojia ya masoko kwa maana ofisi hazitaajiri maofisa masoko hivyo kazi zote zitafanywa na teknolojia ikihusisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) ambayo itaendeshwa na AI.

Tayari baadhi ya application hizi zitaanza kuwapo kwenye kampuni mbalimbali kuanzia mwakani, kampuni kubwa duniani zaidi ya 200 tayari zimetuma maombi ya kupata Apps hizi ili kuimarisha huduma kwa wateja wao.

Uwezo zaidi pia umeelekezwa kwenye ndege za Drones, Roboti na magari yanayojiendesha yenyewe ambapo inaelezwa kuwa kila kimoja hapo kitajumuishwa kwenye matokeo makubwa ya masoko na kuhakikisha kuwa inasaidia kukuza biashara kwa haraka zaidi duniani kote.

Hata hivyo, yote haya yatafanyika kwa kuwapo na intaneti yenye kasi ya kufanya vitu au Internet of Things (IoT) ambapo vifaa kama simu zitakuwa zimeunganishwa na mifumo yote ikiwamo ya ofisini, nyumbani, hospitali na maeneo yote yanayogusa maisha yako.

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri ni wazi kuwa utakuwa umeona mfano wa maisha yanakoelekea kupitia teknolojia moja ya roboti wa kike iliyotengenezwa nchini Japan ambayo inakupa taarifa zote na kukukumbusha mambo unayotakiwa kufanya na kwa wakati gani.

Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, mabilioni ya vitu yanatarajiwa kufanywa na teknolojia ikiwamo ya Digital Twins, hii ni software ambayo inabadilika kulingana na kitu halisi ambapo ina uwezo wa kukibadilisha kitu chako halisi na kukiongezea thamani maradufu kwa kutumia uhalisi wa taarifa zako ikijumuisha taarifa (data) na sensa na kuzipeleka unakotaka wewe duniani. Kwa hali hii, kuna hatari ya watu wengi kupunguzwa kazi!

Je, umejiandaaje kwa hili? 0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles