24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TCU yakifungia chuo kingine cha Mtakatifu Joseph

MgayaNA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza tena kufuta kibali kilichoanzisha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania (SJUIT) tawi la Arusha.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita kufuta vibali vya vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph vinavyomilikiwa na Shirika la Kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alizitaja sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya muda mrefu baina ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji wake kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.

“Kwa kipindi hiki chote tume imekuwa ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki ikiwamo kutoa maelekezo kwa uongozi wa chuo kurekebisha kasoro zinazousababisha.

“Hata hivyo, jitihada za TCU kukitaka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph  kampasi ya Arusha kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa lakini hazikupewa uzito stahiki na uongozi wa chuo,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema chuo hicho kilikuwa na jumla ya wanafunzi 1,557 wanaosoma programu za masomo ya ualimu wa sayansi.

“Kutokana na changamoto hizo, Tume imejiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya chuo hicho imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu,” alisema Profesa Mgaya.

Kuhusu wanafunzi waliokuwa wanasoma katika chuo hicho kilichofutiwa usajili alisema wameidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote wa chuo hicho kwa gharama zote za chuo hicho na orodha ya majina yao na vyuo watakavyopangiwa vitatangazwa na kuwekwa katika tovuti ya TCU.

Pia alisema wamefuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi na wanafunzi wanaoendelea na masomo katika programu hiyo watahamishiwa katika kampasi ya chuo hicho iliyopo Luguruni, Dar es Salaam.

“Wanafunzi hao watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya diploma kama ilivyokuwa imeanishwa na TCU hapo awali. Utaratibu wa uhamisho wa wanafunzi wa programu hii utatangazwa hivi punde na kuwekwa katika tovuti ya TCU,” alisema Profesa Mgaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles