23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

TCAA yaanzisha mfuko wa mafunzo ya urubani

*Lengo ni kuchochea marubani wazawa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kutokana kuwepo kwa uhaba wa Marubani nchini, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeanzisha mfuko wa mafunzo ya marubani ili kuweza kupata marubani wazawa watakaotosheleza kwenye soko.

Akizungumza leo Julai 5, jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea banda la TCAA kwenye maonyesho ya 47 ya biashara Sabasaba ,Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema wameanza kusomesha marubani ili kupunguza changamoto waliyonayo ya uhaba wa marubani hasa wazawa.

Amesema pesa za kuwalipa marubani ni nyingi na marubani waliopo ni wachache hali inayosababisha rubani kufanya kazi zàidi ya kampuni moja.

“Katika sekta yetu tunachangamoto kubwa mbili ambazo ni uhaba wa marubani pamoja miundombinu ya viwanja vya ndege katika kuliona hilo tumeanzisha mfuko wa mafunzo ili wakimaliza waajiriwe na kupunguza changamoto hiyo,” amesema Johari.

Amesema wananchi kwa kutopenda masomo ya sayansi ndiyo imekuwa chanzo cha upungufu wa marubani, hivyo wameanzisha Club za kuhamasisha wanafunzi ili kuwajengea uwezo.

Katika hatua nyingine, amefafanua zaidi kuwa wamevifungia viwanja vya ndege 300 kwa kutokuwa na vigezo vya kurukia ndege, amesema viwanja hivyo hasa ni vile vilivyopo kwenye mapori.

Ameongeza kuwa TCAA ndio wenye mamlaka ya kusimamia ujenzi wa viwanja vya ndege pia na huduma za ardhini zikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za chakula ujazaji wa mafuta.

“Kuna kampuni zinatoa huduma za adhini kama Swissiport sisi ndiyo tunawapa kibali cha kutoa huduma hizo,” amesema Johari.

Aidha, ameongeza kuwa TCAA inatoa leseni kwa ndenge nyuki (droni) ambapo mtoa huduma husika anapaswa kuwa amesajiliwa na kupatiwa leseni .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles