21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

TBA yaahidi kuendelea kubuni na kutekeleza miradi kwa ufanisi

Na Yohana Paul, Geita

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wamewahahakikishia Watanzania kuwa wataendelea kubuni, kutathimini, kutekeleza na kusimamia miradi ya ujenzi kwa ufanisi kwani Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa TBA kuwajibika.

Meneja Uhusiano kwa Umma wa TBA, Fredrick Kalinga amesema hayo kwa waandishi wa habari katika Maonyesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita.

Amesema tayari Serikali imeshafanyia kazi changamoto zilizokuwepo TBA ikiwemo uhaba wa watumishi, vitendea kazi na hivo wana uhakika miradi yote wanayosimamia inakamilika kwa wakati.

“Pale katika mji wa serikali Mtumba Dodoma tumefanya mradi wa majengo ya serikali na wizara 28, ambapo moja ya jengo hilo ni ofisi za wizara ya madini, ambapo kwa sasa tunafanya usimamizi na mradi huo umefikia asilimia 58 ya mradi.

“Tuna majengo matatu ambayo tumeyajenga katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita, lakini tuna majengo matano ambayo tumeyajenga katika hospitali ya rufaa ya kanda Chato na majengo sita ya ofisi mbalimbali hapa mkoani Geita.

“Vilevile tuna mradi mkubwa wa nyumba za watumishi 3500 pale Nzuguni Dodoma, ambapo hapa tumekuwa tukiwaonyesha wananchi pamoja na atumishi ambao wanafanya kazi na wamekuwa na shauku la kuona mradi huo,” amesema.

Ameongeza:“Tuna watalaamu wa kutosha, tuna wataalamu ambao wana ajira za kudumu serikalini, lakini vile vile tulipata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kuajiri wafanyakazi wengine kwenye miradi kwahiyo imetuongezea nguvu ya kutekelza majukumu yetu,”.

Amesema TBA chini ya Wizara ya Ujenzi tayari wamekamilisha ununuzi wa mitambo muhimu na ujenzi wa viwanda viwili vya kuzalisha raslimali ujenzi ikiwemo tofari na zege vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles