Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikieleza kufanyika kwa uharibifu na uvamizi wa mifugo ndani ya mapori ya akiba ya Liparamba na Selous.
Akitoa taarifa hiyo leo Jumanne Novemba 9, Afisa Habari Kitengo cha Uhusiano kwa Umma, Beatus Maganja, alikemea vikali upotoshaji huo uliosambazwa mitandaoni na kuwataka wananchi wazipuuze.
Alisema katika taarifa hiyo ambayo ilieleza kutokana na ziara ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro (Mb) mkoani Ruvuma haikutaja ilifanyia lini huku ikiambatanishwa na picha ya kiongozi huyo.
“TAWA inapenda kuufahamisha Umma kuwa taarifa hizi zinazosambazwa hasa katika mtandao wa twitter ya mtu aliyejitambulisha @HakiNgowi picha na taarifa anayoambatanisha si za maeneo tajwa,'”amesema.
Maganja amesema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kusambaza taarifa za kweli zenye maslahi mapana kwa taifa na wapende kufuatilia vyanzo sahihi vya habari