32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAWA YACHANGIA UJENZI HOSPITALI YA SERENGETI

Na Elia Mbonea, Arusha

Wananchi na wadau wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuchangia mradi wa ujenzi wa majengo ya Hospitali ya kisasa ya wilaya kwa kutoka mchango wa Sh 1,000.

Akizungumza na MTANZANIA DIGITAL wilayani hapa Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu alisema, bado wanaendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau na wananchi.

“Kwenye mikutano ninayoifanya na wananchi nimekuwa nikiwasisitiza kujitoa kwa kauli mbiu ya “Jenga Hospitali kwa Sh 1,000.” Tuna vijiji 78 nimefanikiwa kutembelea vijiji vitatu na kukusanya Sh Milioni 10,” alisema Babu na kuongeza:

“Hivyo ndivyo tunavyotafuta fedha nia yetu kila mwananchi wa Serengeti tunataka awe na uchungu na hospitali hii kwa kuweka Sh 1,000 yake kwenye ujenzi ili tukijaliwa tuifunge Februari mwakani,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya na Katibu wa ujenzi wa Hospital Kamala Cosmas Kamala alisema, awai walihitaji Sh bilioni 1 kwa ajili ya kumalizia jengo moja la hospitali ili ianze kufanya kazi.

“Tulijiuliza hizo fedha tutazisubiria mpaka lini kutoka serikalini, tulitafuta mbinu na kuita wadau wa maendeleo Serengeti waliotuchangia na kupata mifuko ya saruji zaidi ya 1,000 iliyotuwezesha kuanza kupiga plasta,” alisema Kamala.

Mbunge wa Jimbo Serengeti (Chadema), Marwa Rioba Chacha alisema gharama ilitumika katika kuendelea kukamilisha baadhi ya maeneo imekuwa kidogo kutokana na kutumia mafundi wa kawaida badala ya kuajiri makandarasi.

Naye Afisa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori TAHA Suleiman Keraryo alisema jengo hilo limechangiwa na fedha zilizotoka kwenye Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya IKONA WMA.

“Tunaposema uhifadhi kwa manufaa ya watanzania wote ni hii kwamba uhifadhi endelevu kwa manufaa ya wananchi TAWA imeweza kutoa mgawo wa fedha kwa Sh milioni 600 kama alivyosema Mkuu wa wilaya zilizotokana na utalii wa picha na uwindaji katika Pori la Akiba la Ikorongo- Grumet,” alisema Keraryo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles