23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Tasilima abeba mikoba ya Lipumba

Na Mwandishi Wetu

BARAZA  Kuu la Chama cha Wananchi (CUF),limeunda kamati ya watu watatu ambao wataongoza chama hicho kwa muda wa miezi sita.

Akitoa taarifa ya maazimio ya baraza hilo lililokutana mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa CUF, Abdul Kambaya, alisema baraza hilo litaongozwa na mwenyekiti wa muda, Twaha Tasilima.

Alisema Tasilima atasaidiwa na wajumbe wawili ambao ni Aboubakar Khamis Bakari na Severine Mwaijage.

“Kamati hii ndiyo itaongoza chama kwa muda wa miezi sita, kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba,”alisema Kambaya.

Alisema katika muda huo, kamati hiyo itakuwa ikishirikiana kwa karibu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Tasilima, amekabidhiwa jukumu hilo ikiwa ni siku chache baada ya Profesa Lipumba kujiuzulu kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kumpata mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katika mchakato huo, Ukawa kwa kauli moja wamempitisha Edward Lowassa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles