Na Anna Ruhasha, Geita
Wamiliki, watumiaji na wasimamizi wa vyombo vya majini wamekumbushwa kufuata sheria zilizowekwa wakati wa utumiaji wa vyombo hivyo hasa kutumia makoti yanayo akisi mwanga ili panapotokea ajari za majini iwe rahisi katika uokoaji.
Wito huo umetolewa na ofisa wa Shirika la Uwakala wa meli Tanzania mkoa wa Geita (TASAC )Rashid Katonga wakati akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya Nne ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.
Aidha amesema shilika hilo lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge ya mwaka 2017, lilianzishwa kutoka na mgawanyiko wa SUMATRA, kutokana na sheria hiyo amesema ilipelekea TASAC kuanza kutoa huduma za utendaji katika kutekeleza shughuli za utendaji, ulinzi na usalama wa usafirishaji majini.
Pia Katonga ametaja shughuli zinazosimamiwa na TASAC kuwa ni huduma za madini, Vipuli, Mitambo, Vilainishi, Mafuta, Nafaka pamoja na Gesi.
“TASAC inafanya kazi katika mikoa inayopakana na ziwa au bahari ambapo tupo mkoani Geita, Mwanza, Musoma, Kigoma, Katavi, Dar es Salaam, Pwani, Rukwa, Lindi na baadhi ya mipaka hapa nchini ikiwamo Holili,”amesema.
Amesema, mkoa wa Geita unatumia vyombo vingi vidogo vya majini ikiwamo mitumbwi na boti vinavyosafirisha abiria na siyo meli ambapo amewataka watumiaji kuzingatia sheria ya matumizi kwa abiria kutumia jaketi linaloasiki mwanga wakati wa safari nakusisitiza lazima ziwezimekidhi viwango, kwa kuhakisi mwanga, pia ziwe na filimbi na mikanda ili iwe raisi katika ukoaji pindi panatokea ajari ya majini.