24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

TARI Naliendele yawapiga msasa Maafisa Ugani kuhusu matumizi sahihi ya viuwatilifu

Na Hadija Omary, Lindi 

TAASISI ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI Naliendele) imeanza kutoa mafunzo kwa Maafisa ugani wa Mkoa wa Lindi juu ya matumizi sahihi na salama ya viuwatilifu lengo likiwa kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la korosho

Utoaji wa mafunzo hayo ni moja ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack alilolitoa hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao hilo kilicholenga kujadili mwongozo wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku za zao hilo kwa msimu wa mwaka 2022/2023.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano kutoka Taasisi hiyo, Emmanuel Mgimiloko amesema mafunzo hayo yanafanyika kila Wilaya ambapo jana Juni 8, 2022 yameanzia wilayani Liwale kwa kuwakutanisha Maafisa Ugani katika shamba la mfano ambapo wameweza kukumbushwa aina za magonjwa ya mikorosho, utambuzi wa wadudu wahalibifu, matumizi sahihi na salama ya viuwatilifu, vifaa kinga pamoja na namna ya kutumia pampu za kupulizia viuwatilifu.

Mgimiloko amesema hatua hiyo imekuja kutokana na kuwapo kwa changamoto ya uwelewa katika uchanganyaji wa viuwatilifu na matumizi sahihi na salama hasa katika kipindi hiki ambacho kwa mujibu wa kalenda ya zao hilo wakulima kutakiwa kuanza kupulizia viuwatilifu katika mashamba yao.

Mgimiloko ameongeza kuwa baada ya Maafisa Ugani hao kupatiwa mafunzo hayo watatakiwa kuyafikisha elimu waliyopatiwa kwa wakulima moja kwa moja sambamba na kufuatilia ili kutoa ushauri na msaada wa haraka panapotokea changamoto katika zao hilo.

Kwa upande wake, Mtafiti kutoka TARI Naliendele, Bobnoel Asenga amesema miongoni mwa changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili maafisa ugani hao wa wilaya ya Liwale ni michanganyo mbali mbali ya viuwatilifu vya magonjwa na wadudu katika zao hilo la Korosho

“Awali, maafisa ugani hawa walikuwa na dhana kwamba mkorosho mkubwa unatakiwa kupulizwa kiwango kikubwa cha kiuwatilifu ukilinganisha na mikorosho midogo yaani kwa mfano unapuliza viuwatilifu vya wadudu waalibifu mbu wa mikorosho na minazi ambapo mkorosho mdogo upulize ml. mbili wakati mkorosho mkubwa upulizwe kwa ml. tano jambo ambalo siyo sahihi,” amesema Asenga.

Aidha, amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo wameweza kuwafundisha maafisa ugani kwamba viuwatilifu hivyo vinapambana na mbu wa mikorosho na minazi na sio ukubwa wa mikorosho kama walivyodhani.

Ameongeza kuwa kwa kutofautisha ujazo wa dawa kwa kulinganisha ukubwa wa mikorosho wadudu wasumbufu hawataweza kufa kwa matumizi hayo bali atazimia na badae kuzuka na kuendelea kushambulia mikorosho kwa kasi mpya.

Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Liwale, Judith Nguli amesema kuwa mafunzo hayo yamefika wakati muafaka kwa kuwa leo Juni 9, ndio wanaanza rasmi ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa zao hilo hivyo yatachochea uwezeshaji kwa maafisa ugani hao wa namna ya wakulima kuweza kuhudumia mashamba yao na baadae kuongeza tija ya uzalishaji katika wilaya hiyo

Hata hivyo, Nguli amewataka wakulima kuacha kutumia viuwatilifu kwa mazoea na badala yake kubadilika ili kuendana na maelekezo ya wataalam katika kuongeza tija ya uzalishaji wa korosho

Kwa upande wake, Zuhura Kimbendela ambaye ni mmoja wa maafisa ugani aliepatiwa mafunzo hayoamesema kuwa ameongeza uelewa wa matumizi ya viautilifu ikilinganishwa na awali.

Amesema amefahamu utofauti wa matumizi ya viuwatilifu hasa kulingana na ukubwa wa mkorosho na ujazo wa viuwatilifu wakati wa kupulizia hivyo mafunzo hayo yameweza kuwaweka sawa maafisa ugani hao na sasa wametoka na ujumbe mmoja ambao watakwenda kufikisha kwa wakulima katika maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles