21.4 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzanite: Wimbo wa Mbagala umeniharibia njia

TANZANITE 2NA ESTHER GEORGE

MSANII wa Bongo Fleva, Athumani Mwingereza ‘Tanzanite’, ameibuka na kudai kwamba wimbo wa ‘Mbagala’ wa msanii, Nasib Abdul ‘Diamond’, umemuweka katika wakati mgumu tangu alipourudia na kuuita ‘Kafara’.

“Wimbo ule nilitumia mdundo wa wimbo wa ‘Mbagala’ nikauita ‘Kafara’, wimbo huo umenisababishia changamoto nyingi sana ikiwemo ya kutokuaminika kwa wadau wengi wa muziki na hata mashabiki wangu hata ninapotoa wimbo mpya.

“Kwa sasa nafanya muziki wangu lakini katika wakati mgumu kwa kuwa nimekosa kabisa watu wa kusaidia kunirudisha kama nilipokuwa, wengi wao hawaamini kama nina uwezo na kipaji cha kutunga na kuimba mwenyewe lakini pia baadhi ya waliokuwa wakinisaidia wapo kwa msanii huyo hivyo tangu niimbe wimbo huo wamesitisha msaada kwangu,” alieleza kwa masikitiko.

Hata hivyo, Tanzanite amewataka mashabiki wake wamsamehe na wasahau yaliyopita kwa sasa ameamua kusimama mwenyewe bila kutumia mgongo wa mtu kuwa juu kisanii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles