26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Stara Thomas: Bado nipo nipo kwenye ‘Gospel’

stara thomasNA ESTHER GEORGE

MKONGWE katika muziki wa Bongo Fleva, Stara Thomas, ameibuka na kudai kwamba muziki wa injili haujamshinda hivyo ataendelea kuimba Bongo Fleva na Injili kwa kuwa nyimbo zake hazipotoshi jamii.

“Baada ya kukaa vizuri ndani ya Biblia nimeona naweza kufanya Bongo Fleva kwa ajili ya kuelimisha jamii huku nikiendelea kuimba muziki wa injili, cha msingi ni kufuata maadili ya pande zote mbili kwa kuwa sina wimbo wa kupotosha jamii.

“Kingine kinachonipa moyo ni kwamba Mungu aangalii naimba Bongo Fleva au muziki wa injili bali anaangalia matendo yangu yanampendeza yeye ama la,” alifafanua zaidi Stara.

Stara Thomas aliwahi kuimba na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva akiwemo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, AT katika wimbo wa ‘Nipigie’ na wengine wengi lakini pia aliingia katika muziki wa injili na kuwa kimya kwa muda mrefu kiasi kwamba mashabiki wake wakadhani ameachana nao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,628FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles