25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tanzania yazidi kunufaika na uwekezaji

Dan Friedkin, Chairman and CEO of Friedkin Companies shaking hands with our President recentlyNa Enock Bwigabe, TUDARCO

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimesema Tanzania imepata uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100 zitakazochangia katika uboreshaji wa utalii na masuala ya uhifadhi nchini.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, ilisema uwekezaji huo ulithibitishwa mwanzoni mwa mwezi huu kupitia Kamati ya Uendeshaji ya Uwezeshaji ya Taifa (NISC) iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uwekezaji huo unaotoka Marekani, ulitokana na juhudi za Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake katika kuitangaza Tanzania kama eneo linalostahili katika uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki, alisema katika taarifa hiyo, kwamba mwekezaji wa Marekani, Shirika la Familia ya Uhifadhi ya Friedkins (FCF) wanakaribishwa nchini na Serikali kwa kuwa inatambua uwekezaji binafsi wa nje na ndani kama chachu ya ukuaji wa uchumi.

“Hii ni tuzo ya pili ya hadhi ya uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya utalii na uhifadhi wa wanyamapori kwa kipindi cha miaka miwili.

“Tuna imani juhudi za kuhamasisha uwekezaji zinazofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na timu yake, itazaa matunda kwa uwekezaji zaidi nchini.

“Kwa uwekezaji huu, tutashuhudia ajira, uhifadhi wanyamapori, maendeleo ya utalii, maendeleo ya kijamii vijijini, maendeleo ya miundombinu na uvumbuzi katika maeneo ambayo kwa sasa yanaingiza idadi isiyoridhisha ya watalii kama vile ukanda wa utalii wa magharibi.

“Cha muhimu zaidi ni kwamba, katika mahali ambapo kuna uhaba wa wanyamapori, uwekezaji huu utaweza kuanzisha utamaduni na utalii wa picha kama njia ya kuvutia rasilimali katika maeneo hayo.

“Kwa kuwekeza, FCF itafanya kazi kwa karibu na idara ya wanyamapori Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuanzisha mikakati dhidi ya ujangili na itaendelea kufadhili na kuendesha mfumo wa habari wa kijiografic (GIS) kwa kupanga na kutafiti juhudi za kupambana na ujangili,” alisema Kairuki katika taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles