Samia: Toeani taarifa za wageni msiowajua

0
2720

Samia Suluhu HassanNA SARAH MOSSI, MZUMBE

 

MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuwa walinzi katika maeneo wanayoishi, ili kuwabaini wageni wanaoingia kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Samia alitoa kauli hiyo jana,  alipokuwa akizungumza na wananchi  wa Kata ya Mlali katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.

Alisema Serikali, imejipanga kuimarisha ulinzi kabla ya siku ya uchaguzi ili kuhakikisha amani inaendelea kutawala.

“Ulinzi unaanza kwetu wananchi, Serikali imejipanga ili mkapige kura, nawasihi mkiona mgeni yeyote ambaye hamumjui pelekeni taarifa kwa viongozi wenu,” alisema.

Kuhusu  mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu, alisema Serikali imejipanga kuongeza kiwango cha mikopo pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanaipata  kwa wakati ili  wasome vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here