27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yatoa mapendekezo matatu kwenye baraza la ACP

Na Mwandishi wetu, Nairobi

TANZANIA imetoa mapendekezo matatu ambayo  yamekubaliwa katika kikao cha mashauriano baina ya Mawaziri wa Baraza la Nchi za Afrika, Carribean na Pacific (ACP) kilichoanza jijini Nairobi, Kenya. 

Mapendekezo hayo ya Tanzania yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof Palamagamba Kabudi, katika mkutano huo wa 110 wa baraza hilo katika ushirikiano na Jumuiya ya Ulaya ambao utafuatiwa na mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi na Serikali katika Nairobi nchini Kenya.

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na  kutodhoofisha umoja wa ACP hususani katika kipindi hiki ambacho nchi hizo ziko katika majadiliano ya kina na jumuiya ya ulaya kuhusu mkataba mpya wa ushirikiano baada ya mkataba wa sasa unaofikia ukomo Februari mwakani..

Profesa Kabudi ameitaja sababu nyingine kuwa ni kuepuka mivutano isiyo na tija kati ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific na Nchi za Jumuiya ya Ulaya hususani katika nyakati ambazo nchi hizo zinahitaji mshikamano zikiwa zinapita katika  kipindi muhimu cha kujenga uchumi na ustawi wa jamii ya nchi zao.

Alisema majadiliano baina ya nchi wanachama wa ACP ni muhimu ili kupitia upya mkataba wa George Town, ambao ndiyo ulianzisha kundi la ACP na kusainiwa katika Jiji la Goergetown nchini Guyana mwaka 1975.

Nchi za ACP zimekubaliana kufanya mabadiliko makubwa ya mkataba huo ili kujenga umoja wa ACP unaoendana  na mabadiliko ambayo yamejitokeza ulimwenguni na masuala ya kimataifa ambayo yanahitaji mtazamo mpya.

Prof. Kabudi alisema katika muktadha huo wa majadiliano, Tanzania imetoa mapendekezo hayo matatu ambayo yote yamekubaliwa na kuungwa mkono na  nchi zote 79 wananchama wa ACP .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles