31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mkuu awafunda majaji wafawidhi

Na Mwandishi wetu, Arusha

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewataka majaji wafawidhi nchini kuwa na umiliki wa masuala yanayohusiana na kazi zao kwa maslahi mapana ya taasisi na jamii kwa ujumla.

Alisema hayo alipokuwa akifunga rasmi mafunzo elekezi ya siku tano kwa majaji wafawidhi na baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa ‘EAC’ jijini Arusha.

Jaji Mkuu alisema Mahakama ni mhimili wa dola uliopewa dhamana ya mwisho ya utoaji haki na tafsiri ya sheria hivyo kila jaji ama hakimu ana haki na wajibu wa kusimamia dhamana hiyo. 

 “Kama viongozi wa maeneo yenu, mna wajibu wa kusimamia maeneo mbalimbali ikiwemo usimamizi wa sheria, usimamizi wa utekelezaji wa Mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri (JSDS II), kusimamia uadilifu na maadili ya watumishi walio chini yenu.

“Ili kuhakikisha mfumo wa JSDS II unafanya kazi vizuri, ni vyema mkaendelea kutoa mawazo yenu yenye tija  kwa timu yetu ya ndani inayoendelea kutengeneza mfumo huu ili kuwezesha ukufanye vyema,” alisema Jaji Mkuu.

Jaji Prof Juma aliwataka majaji hao wanapotoa huduma kwa wananchi kuhakikisha kiwango cha wananchi wanaotumia huduma za mahakama wanaridhika, na upatikanaji wa taarifa muhimu za kesi na kujiuliza endapo huduma zetu ni rafiki kwa wahudumiwa. 

Awali akimkaribisha Jaji Mkuu kufunga rasmi mafunzo hayo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Eliezer Feleshi, alimshukuru Jaji Mkuu kwa kukubali kufanyika kwa mafunzo hayo yenye mafanikio makubwa.

“Napenda nikushukuru Jaji Mkuu kwa kuridhia kufanyika kwa mafunzo haya na vilevile nishukuru kamati nzima ya maandalizi kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo haya, kitu ambacho nasisitiza ni kuendelea kufanya kazi kama timu moja ili kufanikisha mipango tuliyojiwekea,” alisema Dk Feleshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles