25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapokea dawa ya corona

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

AHADI ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku tano zilizopita kwamba atatuma ndege Mada- gascar kufuata dawa ya mitishamba ambayo rais wa nchi hiyo anadai kuwa inatibu corona, imetimia.

Tayari ndege hiyo ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Ka- budi imekwishawasili nchini Madagascar na kupokea dawa hiyo .

Katika picha zilizoanza kusambaa jana kwenye mitandao ya kijamii kabla ya baadae kuthibitishwa na Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, ilionekana ndege maalumu ya Tanzania ikiwa imefika nchini Madagas- car ikiongozwa na Profesa Kabudi pamoja na ujumbe mwingine.

Picha hiyo ambayo imechapishwa na mtandao wa Orange actu Madagascar ilikuwa na maelezo yanayosomeka kwa lugha ya kiin- gereza; “ Ndege maalumu ya ujumbe kutoka Tanzania imetua Ivato kuchukua msaada ku- toka Madagascar wa dawa ya tiba asili ya virusi vya corona”

Baadae Msemaji Mkuu wa Serikali aliandi- ka kupitia mitandao ya kijamii kwamba; “Tan- zania leo imepokea msaada wa dawa zinazo- fubaza Virusi vya Corona kutoka Serikali ya Madagascar”.

Andiko lake hilo liliambatana na picha za maboksi ya dawa hizo na nyingine zinazomuo- nyesha Profesa Kabudi akipokea dawa hizo ku- toka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mada- gascar Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva.

Picha nyingine ilionyesha hafla fupi iliyo- fanyika nchini humo ya kukabidhi dawa hizo.

Zaidi picha nyingine zilimuonyesha profesa Kabudi akiwa ameshika dawa hiyo na nyingine akiwa anakunywa kwenye glasi.

Uamuzi wa Rais kutuma ndege kwenda kuchukua dawa Madagascar aliusema Mei 3, mwaka huu katika hafla fupi iliyofanyika Cha- to ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki Ijuuma iliyopita. Rais Magufuli mbali na kudokeza yale aliyobaini kuhusu vipimo vya ugonjwa huo pia alizungumzia kuhusu uamuzi wake wa kwenda kuchukua dawa hiyo nchini Madagascar.

Zaidi alisema kuwa amewasiliana na Mada- gascar baada ya kupokea barua rasmi kutoka nchi hiyo iliyoeleza kuwa wamegundua dawa ya corona.

“Ninawasiliana na Madagascar na wame- shaandika barua. Wanasema kuna dawa zime- patikana kule, tutatuma ndege kule na dawa zile zitaletwa pia ili Watanzania nao waweze kufaidika nayo… Sisi serikali tupo tunafanya kazi usiku na mchana.”

Aidha Rais Magufuli alitahadharisha watu kuendelea kuchukua hatua za kujikinga ikiwa ni pamoja na kutofanya safari za lazima.

Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) halijathibitisha juu ya ubora wa dawa hiyo am- bayo ni kinywaji kilichotengenezwa kwa mit- ishamba. Uamuzi wa Rais Magufuli unakuja baada ya Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina

kutangaza kwamba taifa lake limezindua dawa ya mitishamba ya kutibu Covid-19.

KABUDI

Akizungumza wakati akipokea dawa hiyo, Prof. Kabudi amesema madai yanayotolewa kuwa Tanzania imelegalega ama kujitenga ka- tika kupambana na ugonjwa wa COVID 19 si ya kweli kwa kuwa Tanzania imetoa uongozi madhubuti katika eneo iliyopewa dhamana ya uongozi ya Uenyekiti wa nchi SADC na imei- fanya na inaendelea kuifanya kwa heshima na bidii zote.

Ameongeza kuwa Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa SADC tangu kuzuka kwa ugonjwa wa COVID -19 tayari imesimamia na kuratibu mikutano iliyoendeshwa kwa njia ya mtandao (Video Conferencing) kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa huo na kutoa mwon- gozo wa jinsi ya usafirishaji wa bidhaa muhimu na kwamba miongozo hiyo imetolewa na kuku- baliwa na nchi zote wanachama wa SADC

Amesema miongoni mwa masuala wali- yokubaliana katika mikutano ya SADC ni pamoja na kukubaliana kuwa kila nchi ya SADC ichangie aidha katika kutafuta njia ya kusaidia kupunguza nguvu ama kuleta tiba ya COVID – 19 na Madagascar imekuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi wanachama kupiga hatua ndani ya SADC na ndani ya Afrika.

Amesema katika mkutano ujao wa SADC wataitambua Madagascar kwa mchango wake wa kupambana na virusi vya corona.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva amezitaka nchi za Afrika kuungana kwa pamoja kupata suluhisho la maradhi ya COVID 19 ambayo pia itakuwa suluhisho na faraja kwa dunia nzima.

Ameongeza kuwa ni faraja kwa Madagas- car kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kufika nchini humo

kwa ajili ya kujionea dawa hiyo jambo ambalo anaamini kukiwa na nguvu ya pamoja ndani ya SADC ya kuendeleza dawa hiyo na kuifanyia tafiti zaidi itakuwa mkombozi kwa maisha ya watu wengi duniani.

Dawa hiyo ilizinduliwa hivi karibuni kwa jina Covid-Organics, na imetengenezwa kutoka kwenye mmea unaotambulika kama artemisia au kwa lugha nyingine pakanga – ambao ni mo- jawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Dawa hiyo ambayo imepakiwa kwenye chu- pa na kutangazwa kama chai ya miti shamba ilifanyiwa majaribio miongoni mwa watu wasi- ozidi 20 kwa kipindi cha wiki tatu, kulingana na katibu wa rais wa Madagascar, Lova Hasinirina Ranoromaro aliyewahi kuzungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

“Vipimo vimefanyika-watu wawili wame- kwishapona kutokana na tiba hii,” Rajoelina alisema katika uzinduzi wa Covid-Organics uli- ofanyika katika taasisi ya utafiti ya Madagascar- Malagasy Institute of Applied Research (Imra), ambayo ndiyo iliyotengeneza dawa hiyo ya mit- ishamba.

Rais Rajoelina aliagiza wanafunzi wapewe kinywaji hicho kwa kiwango kidogo kila baada ya muda kwa siku.

“Kinywaji cha dawa hii ya mitishamba huonesha matokeo katika kipindi siku saba,” alisema rais huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwataka watu kuitumia kama hatua ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

“Watoto wa shule wanapaswa kupewa kinywaji … kidogo kidogo kwa siku nzima,” ali- waambia mabalozi na watu wengine waliokua wamekusanyika kwa ajili ya uzinduzi wa kiny- waji hicho.

Pamoja na msimamo wake WHO inasema majaribio ya kimataifa yanaendelea kupata tiba yenye ufanisi dhidi ya virusi hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles