30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Mbunge CCM asomewa mashtaka 12 ya uhujumu uchumi

Na SAM BAHARI -SHINYANGA

MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kishapu na Wilaya ya Kishapu Sulei- man Masoud (Nchambi) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga na kusomewa mashitaka 12 ya uhujumu Uchumi.

Akisoma Mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahaka- ma ya Wilaya ya Shinyanga, Ushindi Swalo Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Magreth Ndawala alisema mtuhumiwa anakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu Uchumi.

Mwendesha Mashitaka Ndawala alisema kati ya Mashitaka 12 yanayomkabili mtuhumi- wa Nchambi ni pamoja na kupatikana na silaha 10 na risasi 536 akizimiliki kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashitaka Ndawala alisema,

tuhuma nyingine ni mtuhumiwa kupatikana na nyama mbalimbali za wanyama pori kiny- ume na sheria, na taratibu za nchi.

Mwendesha Mashitaka, Magreth Ndawa- la alikuwa akisaidiana na Waendesha Mashi- taka wa Serikali wengine Michael Jairo na Castory Mwenda.

Wakili wa upande wa mtuhumiwa, Frank Mwalongo hakupata nafasi ya kujibu hoja yoy- ote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi za uhujumu uchumi.

Mbunge huyo Nchambi alikamatwa na Polisi nyumbani kwake Mei 3, mwaka huu na kupatikana na silaha 16 na risasi 536 na nyama za wanyama pori.

Kesi ya mbunge huyo iliahirishwa na itata- jwa tena katika Mahakama hiyo Jumatatu Mei 11, mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles