25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Sweden kushirikiana uchumi

Dk. Servacius Likwelile
Dk. Servacius Likwelile

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

SERIKALI za Tanzania na Sweden zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka minne  kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2019 utakaojikita kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya watu katika nyanja mbalimbali yakiwamo elimu, utafiti, nishati jadidifu na kupambana na umasikini.

Makubaliano hayo yalifikiwa  mjini hapa jana, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile  na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Sweden, Ulrika Modeer.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Dk. Likwelile, alisema     kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2019, Serikali ya Sweden itatoa ruzuku ya fedha za Kiswidi, SEK 5.5 Biln, sawa na Sh trilioni 1.42.

Alisema kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano huo kunatokana na kusaini   mikataba ya fedha.

Fedha hizo zitaelekezwa katika miradi kadhaa ikiwamo kusaidia elimu, maendeleo ya jamii-TASAF, utafiti, nishati, demokrasia, haki za binadamu  na sekta binafsi.

“Ushirikiano huu umelenga kusaidia kujenga mazingira ya maendeleo endelevu na kuwapatia Watanzania maskini fursa za kujikwamua katika umaskini kwa kujipatia ajira na  a kuanzisha biashara za kujipatia kipato ambako vikundi vinavyolengwa zaidi ni wanawake, watoto na vijana,” alisema Dk. Likwelile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles