28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

CAF yakamilisha mipango ya Yanga

Screenshot_2016-06-17-09-48-22

* Kessy, Kakolanya, Mahadhi, Dante kuivaa Mo Bejaia

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameendelea kuwazidi kete wapinzani wao, Mo Bejaia, kuelekea  kwenye mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Jumapili baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwaruhusu  kuwatumia  wachezaji  wapya wanne  kwenye mchezo huo.

Uamuzi wa CAF kuwapitisha wachezaji wapya kipa, Benno  Kakolanya, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew ‘Dante’ na Juma Mahadhi, unatarajiwa kuongeza nguvu na hamasa ya ushindi  kwenye kikosi cha timu hiyo hasa kwa Kessy kuziba nafasi ya Juma Abdul aliyebaki nchini kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu ‘enka’ yanayomsumbua.

Yanga ambayo iliweka kambi katika Hoteli ya Rui mjini Antalya, Uturuki tangu Jumapili iliyopita inatarajia kutua Jiji la Bejaia leo vilipo  viwanja vya Unite Maghrebine nchini Algeria  kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deosdedit, alisema  uamuzi wa CAF  wa kuwapitisha wachezaji hao unamaana kubwa kwenye kikosi chao ambacho kitashuka dimbani Jumapili hii kukabiliana na wapinzani wao, Mo Bejaia.

“Kwa sasa tunakila sababu ya kushinda si mchezo huo wa Jumapili pekee, bali michezo yote  ya Shirikisho  iliyopo mbele yetu kutokana na kikosi chetu kuongeza nguvu mpya.

“Wachezaji wote wapo salama na wanatarajia kesho (leo) kutua Algeria kwa ajili ya mchezo huo ambao utachezwa usiku,” alisema Deosdedit.

Naye Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema  kwamba  leseni za wachezaji hao ili kucheza michuano hiyo  ziliwasili juzi  kutoka CAF.

“CAF imetuma leseni za wachezaji hao wanne wapya wa Yanga na maana yake sasa wako huru kucheza Kombe la Shirikisho.

“Wachezaji hao wanaweza kutumika kwenye mchezo huo na mingine ya Shirikisho kutokana na leseni hizo kuwaruhusu,” alisema Lucas.

Taarifa  kutoka nchini Algeria zinadai kwamba mchezo huo unatarajiwa kuchezwa usiku saa 22:15, huku tiketi zikianza kuuzwa siku hiyo ya mchezo saa 11:00 asubuhi.

“Mashabiki wataanza kuingia  saa 2:30 usiku kwa kiingilio cha Sh 5,830  fedha za Kitanzania kwa jukwaa la kawaida, huku jukwaa la kati wakilipa  Sh 9,718 , fedha za Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.

Baada ya mchezo huo, Yanga imepanga kurudi tena nchini Uturuki kuendelea na mazoezi tayari kujiandaa na mchezo wake dhidi ya TP Mzembe ya DR Congo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles