Na Mwandishi wetu
Tanzania imetengeneza nafasi muhimu katika biashara Afrika kutokana na uhusiano na mataifa mengi ulimwenguni, hivyo kuwa na uwezo wa kupata nafasi ya uwanzilishi wa ukuaji wa viwanda na kuhakikisha fursa hiyo inakua.
Akizungumza jana Desemba 10, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya EnergyNet, Simon Gosling amesema Tanzania ni eneo muhimu kwa shughuli za uwekezaji barani, ambapo inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa tano wa mwaka wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit( TECS) unatarajia kufanyaia Januari 31 hadi Februari mwaka 2024 jijini Arusha.
“Kwa kuzingatia nafasi ya Tanzania kama mhimili wa nishati kikanda, mada zitakazojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na mtazamo wa kiuchumi wa Tanzania na uwezo wa maendeleo ya nishati pamoja na kupanga njia bora ya kujenga soko la umeme kikanda,” amesema Gosling.
Amesema kuona ukuaji wa pato la taifa kwa asilimia 6 ifikapo mwaka 2025, huku ikishudia mamilioni ya uwekezaji wa dola unaolenga kuwekeza kwenye miundombinu, maji, umeme na gesi asilia (LNG) na miradi ya nishati ya jua kati ya miaka ya hivi karibuni.
Amesema ni Taifa lililotwajwa kwa eneo lake la kimkakati mashariki mwa barani Afrika kwa wingi wa maliasili na ongezeko la uwekezaji hivi karibuni katika sekta ya nishati.
Amesema mkutano huo wa wa TECS24 umeratibiwa na Energy Net hautoainisha mafanikio hayo ya kujivunia pekee bali itaangazia fursa zijazo za biashara na miradi ya uzalishaji inayotarajia kubadilisha nchi na ukanda huo zaidi.
Ameeleza changamoto zinazohusiana na fedha na dhamana pia zitajadiliwa ili kuchochea ari zaidi ya majadiliano na kuhakikisha sekta ya umeme nchini inaendelea kuimarika zaidi.
“Ushirikiano wa sekta za umma na binafsi katika miradi ya usafirishaji pia utakuwa kwenye ajenda pamoja na wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha utawala na kanuni na nafasi muhimu ya nishati mbadala na washiriki watapewa fursa ya kutoa mawazo na kuweka mifumo imara zaidi katika biashara na uwekezaji, “amesema.
Aidha Gosling amesema wawekezaji kutoka sekta mbalimbali za fedha na serikali zitakutana kuonyesha uwezo mkutano huo.
Naye Mkuu Mwenza wa ‘Infrastructure Sector Group Afrika’, Aleem Tharani amesema mkutano huo wa tano wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit unaweka alama muhimu kwa sekta ya nishati barani Afrika.
“Kwa kuwaunganisha wawekezaji, taasisi za serikali na watalaamu wa sekta, tunachochea majadiliano muhimu kwa ajili ya kukuza ramani ya nishati ya Tanzania, kutoa kipaombele kwa gesi na nishati mbadala na kuboresha usafirishaji wa kikanda, ” amesema Tharani.