Na Mwandishi Wetu
BALOZI wa Tanzania Nchini Algeria, Iman Njalikai leo Oktoba 30, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Noureddine DJoudi, Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha Ukombozi ambaye ndiye Balozi wa Kwanza wa Nchi hiyo nchini Tanzania baada uhuru mwaka 1962.
Mazungumzo na balozi huyo yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers na yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Algeria na Tanzania.
Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na Serikali .
Katika kumhakikishia ushirikiano zaidi Balozi Njalikai amemshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya ubalozi na mamlaka mbalimbali za Algeria ikiwemo sekta binafsi.
Kwa upande mwingine, Ubalozi umepokea na unafanyia kazi ombi la Balozi Joudi kuhusu kuimarisha kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini ikiwa ni pamoja na kuitangaza zaidi Lugha hiyo kwa kuifundisha wa Algeria