Na ASHA BANI
“MWAKA 2016 ni siku ambayo sitaisahau maishani mwangu kwa furaha niliyoipata baada ya kusikia kuwa nimeteuliwa na Rais John Magufulikuwa mkuu wa wilaya ya Busega.
“Nilijua moja kwa moja ndoto yangu imetimia, namshukuru Rais kwa kuniamini na kuniteua katika nafasi hii muhimu ya kuwahudumia Watanzania hasa wakazi wa Busega,” hivi ndivyo anavyoeleza Mkuu waWilaya Busega, Tano Mwera.
Alisema nafasi hiyo ameipata wakati mwafaka, ambao alikuwa na kiu ya kufanya mambo mengi kwa ajili ya kuisaidia nchi yake hasa katika maendeleo.
Hata hivyo alieleza kutopata changamoto zozote pindi alipofika
kuripoti na kuanza kuchapa kazi kwani aliamini wanaBusega wanategemea
maendeleo
“Lakini kwa kawaida huwezi kukubalika na kila mtu, wapo pia wanaoshangaa kuona Mkuu wa Wilaya mwanamke kwani walizoea kuona wakuu wa wilaya wanaume, lakini
sasa wameelewa tunaenda vizuri tu na tunachapa kazi za kuleta
maendeleo,’’alieleza Tano.
Malengo
Akizungumzia malengo ya Kiwilaya katika utendaji wake kwa mwaka 2017/2018 alisema lengo ni kukuza elimu na tayari ameanza kuongeza vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule kwani tangu Sera ya Elimu Bure ianze uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka na wanaofaulu wameongezeka hivyo kuna jukumu kubwa la kuongeza vyumba vya
madarasa na ikibidi shule mpya.
“Ni lazima kuongeza shule mpya maana huko tunakokwenda italazimika sasa kila kata kuwa na sekondari mbili badala ya moja na pia kuweka mikakati ya kukuza shughuli za uzalishaji katika sekta ya mifugo, kilimo, uvuvi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili vijana wapate ajira na kuondokana na umaskini sambamba na kuanzisha mradi wa umwagiliaji mkubwa katika kata ya Mwamanyili,’’alisema Tano.
Alisema wilaya hiyo ina jumla ya watu 203,597 kwa mujibu wa
sensa ya mwaka 2012 huku akazi wake wengi wakitegemea kilimo na uvuvi .
Historia
Alianza shule ya Msingi mwaka 1981 na kumaliza mwaka 1987 katika shule ya Msingi Mkongo iliyopo Rufiji, Mkoa wa Pwani na kufaulu katika shule ya wasichana wenye vipaji maalumu ya Tabora Girls kuanzia mwaka 1988 mpaka 1991.
Alisema alifanya vyema pia na kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga kwendakatika shule ya wasichana wenye vipaji maalumu ya wasichana ya Msalato Mwaka 1992/1994.
“Baada ya hapo nilifanya kozi fupi ya ‘front office Management’ na kuniwezesha kufanya kazi , White Sands Hotel kama telephone operator na baadaye British Council kama telephone operator/ secretary.
“ Mwaka 2001 nikajiunga Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuchukua Advance Diploma ya Information Communication (ICT) kipindi ambacho pia nilikuwa nafanya kazi Wakala wa Barabara (TANROADS) kama mtu wa
mapokezi na msaidizi wa rasilimali watu,’’alieleza Tano.
Alisema mwaka 2005 alimaliza IFM ambapo
mwaka 2007 alisomea Diploma ya Rasilimali watu katika chuo cha kifahari kiitwacho Varsity College kilichopo Mjini Cape Town.
“ Mwaka 2008 nikajiunga na Cape Peninsular University of Technology kusoma, BTECH Degree ya Business Administration na mwaka 2010 nikajiunga na University Of The Western Cape kuchukua Master Degree ya Public Administration.
“ Nikiwa Afrika Kusini nilifanya kazi katika sehemu mbali mbali ikiwamo 121 Group ni Call Centre Company, TAC – Treatmen Action Campaign NGO kubwa mjini hapo inayopigania haki za matibabu kwa watu
wenye maradhi ya ugonjwa wa Ukimwi (HIV),’’alisema Tano.
Historia katika siasa
Kiilichomhamasishsa kuingia katika siasa ni kutokana na msukumo na kuguswa na matatizo ya jamii yake.