27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANGAWIZI SI KIUNGO TU, BALI PIA NI TIBA


Na Fadhili Paulo

TANGAWIZI ni kiungo kinachotokana na mizizi ya mmea wa tangawizi.

Mmea huu unafanana na binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Kwa hapa Tanzania, hulimwa zaidi katika mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro na kwingineko.

Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au hata kwa kilo. 

Tangawizi inatumikaje?

Mmea huu unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea, lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa unga.

 Faida zake

Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.

Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa wagonjwa hasa walio athirika na ugonjwa wa Ukimwi. Hivyo, kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya maajabu ya mmea huu. 

Jinsi ya kutumia kama dawa

Tangawizi ikiwa imesagwa au mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia ni katika chai, inakuwa ni mbadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffein inayosababisha magonjwa mengi mwilini. Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katia juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.

 Hutibu magonjwa gani?

Tangawizi inaweza kukusaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu

kutapika, kuharisha, kisukari, shinikizo la damu, kuongeza msukumo wa damu na kutoa sumu mwilini.

Matatizo mengine yanayoweza kuondoka kwa kunywa tangawizi ni maumivu ya tumbo na gesi tumboni.

Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia kutuliza au kuondoa kabisa mafua au flu na magonjwa mengine mengi.

Mwandishi wa makala hii ni tabibu wa tiba asilia, kwa maswali na ushauri wasiliana naye kupitia WhatsApp +255769142586.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Tangawizi kweli ni dawa lakini kuna usemi watu wanatumia utkitumia tumbo halina kitu ina madhara je ni kweli?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles