Na MWANDISHI WETU - KIDATU -
KUTOKANA na umeme wa maji (Hydro power) kuwa wa gharama nafuu zaidi ikilinganishwa na unaotokana na vyanzo vingine, Serikali imepongezwa kwa kulinda vyanzo vya maji.
Akizungumza hivi karibuni, Naibu Mkurugenzi wa Tanesco anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema matumizi ya juu ya umeme nchini kwa sasa ni megawati 1,060.
Alisema kati ya hizo, Tanesco kwa kutumia mitambo yake, huzalisha megawati zaidi ya 1,000 ambazo megawati 381 zinatokana na umeme unaozalishwa kutokana na maji, kutoka katika vituo vya Kidatu, Mtera, New Pangani Falls, Hale na Nyumba ya Mungu.
Alisema katika siku za hivi karibuni, shughuli za kibinadamu zimekuwa zikiongezeka kwenye vyanzo vya maji na kuathiri vituo vya kufua umeme na hata kutishia uzalishaji.
Ikwasa alitoa mfano Mto Pangani ambako yapo maeneo ambayo shughuli za kilimo zinaendelea karibu na mto, na madhara yatokanayo na shughuli hizo husababisha kingo za mto kuwa dhaifu na wakati wa mvua maji yanachukua udongo na kuingiza kwenye mto na hivyo kina kinakuwa kifupi.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.