26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

MWANDISHI AZAM TV AFARIKI DUNIA

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA mpigapicha wa Kituo cha Runinga cha Azam, Idd Mambo (34), amefariki dunia baada ya kuugua ghafla akiwa safarini jijini Mwanza alikokwenda kikazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhai Production Ltd, Tido Mhando, alisema Mambo alifariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikopelekwa kwa matibabu.

Alisema akiwa huko, alishikwa na maradhi ya tumbo na ikabidi afanyiwe operesheni ya haraka.

“Alikuwa mpigapicha hodari tuliyekuwa tukimtegemea sana,” alisema Mhando.

Mwili wa marehemu uliwasili Dar es Salaam jana mchana kwa ndege na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Kawe, Wilaya ya Kinondoni.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles