23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CUF LIPUMBA KUMVUA UANACHAMA MTATIRO


Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif, Julius Mtatiro na wenzake huenda wakavuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukaidi wito wa kamati ya utendaji ya chama hicho.

Wanachama hao waliitwa na Kamati ya Utendaji ya CUF Wilaya ya Ubungo kujibu tuhuma kwanini wasifukuzwe kutokana na mienendo yao ndani ya chama hicho.

Mbali ya Mtatiro wengine ni Khalid Singano, Kassim Choga, Mawano Yusuf Kilemi, Jumanne Ally, Mwinyi Khamis na Twaha Rashid.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu wa CUF Wilaya ya Ubungo, Ali Makwilo, alisema kikao hicho kilifanyika jana lakini waliotikia wito huo ni wanachama wawili tu.

Aliwataja wanachama walioitikia wito huo kuwa ni Katibu wa Tawi la Kimara Stop Over, Yahaya Muhsin na Katibu wa Tawi la Matangini, Patrick Mwakasege.

“Ni kweli tumewaita na wapo waliokuja lakini Mtatiro na wenzake hawakuja, maana yake wamedharau wito. Kisheria ukituhumiwa halafu hukwenda unaruhusu mamlaka ikuadhibu.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles