28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA wamlilia Sara Dumba

DSC03707Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe na mwanachama wao, Sara Dumba ambaye alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia jana wilayani Njombe.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga ilisema wanaungana na familia na Watanzania wote kutokana na kifo cha Sarah ambaye wakati wa uhai wake alisifika kwa uchapakazi.

“TAMWA inaungana na familia ya marehemu Sara, Serikali, wanahabari na Watanzania wote kuombeleza msiba, ameacha pengo kubwa kwenye taasisi ya wanahabari hasa wanawake na Taifa kwa ujumla…alifanya kazi zake kwa umakini na weledi wa kuigwa,” ilisema taarifa hiyo.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba amewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania Dar es Salaam- (RTD), Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT) ambayo kwa sasa inajulikana kama Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), huku akivuma katika Kipindi cha Majira na vipindi vingine vingi.

Mwaka 1998, aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Redio Tanzania mkoani Morogoro na baadaye kuhamishiwa Dodoma kabla ya kuteuliwa mwaka 2006 na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na baadaye alihamishiwa wilayani Njombe hadi umauti unamkuta.

Sara Dumba kitaaluma, alisomea mafunzo ya utangazaji  nchini Misri, pia alipata mafunzo kutoka chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es Salaam.

Naye mtangazaji mkongwe na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi alisema Taifa limepoteza hazina ya mfanyakazi asiyekuwa na makuu.

“Namkumbuka Sara alinipokea pale RTD mwaka 1974, nikiwa na mwenzangu Salim Mbonde, alitupatia ushirikiano mkubwa mno katika utendaji kazi wetu. Sauti yake ilikuwa kivutio kikubwa kwa wasikilizaji wetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles