24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA: Sheria irekebishwe kukomesha ajali zinazozuilika

Mkurugenzi Mtendaji-TAMWA, Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji-TAMWA, Edda Sanga

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimelipongeza Jeshi la Usalama Barabarani kwa kuchukua jitihada na hatua mbalimbali ambazo zina lengo la kumaliza tatizo la ajali zabarabarani ambazo nyingi zinaweza kuepukika na kupunguza au kumaliza kuwepo kwa watu wenye ulemavu na vifo vitokanavyo na ajali hizo na idadi kubwa ya watoto yatima na wanawake wanaotaabika na maisha kwa kuachwa wajane.

Mkurugenzi Mtendaji, Edda Sanga,  amesema Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani siku zote limekuwa likiingia katika lawama, hivyo kwa umuhimu mkubwa ulioonekana mara baada ya ajali iliyotokea kijiji cha Nsalala mkoani Shinyanga, ambapo gari ndogo ya abiria aina ya Noah lenye namba za usajali T 232 BGR lililogongana uso kwa uso na lori na kuua watu 19, ambapo kati ya hao, wanawake walikuwa 10, watotowa kike 3 na wanaume 6, uzembe ambao usingeachiwa bila kuchukuliwa hatua.

“TAMWA kama moja ya wadau wa kuu wa masuala ya usalama barabarani inaunga mkono uamuzi uliotolewa wakuvuliwa  nyadhifa kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoaniTabora (RTO) Shida Machumu na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Bararani wilaya ya Nzega (DTO), Thomas Sengecha pamoja na maaskari polisi wa kikosi cha barabarani wengine 6, ambao walionekana kutokuwajibika mapema kuchukua hatua za kuzuia ajali hiyo ya NOAH,” alisema Sanga

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Fortunatus Muslim, uamuzi huo wa Jeshi la Polisi umechukuliwa baada ya uchunguzi wa  kina kufanyika.

Uchunguzi ulibaini kuwa abiria 21 walipakiwa katika NOAH hiyo pasipo kuchukuliwa hatua zozote na askari wa eneo hilo ambapo kwa kawaida gari ya aina hiyo hutakiwa kupakia idadi ya abiria 8.

Sanga alisisitiza kuwa ni nidhahiri kuna uzembe ulifanyika ambao umetokana na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa baadhi ya askari kwa kutumia mamlaka walizopewa.

“Sambamba na pongezi hizi kwa jeshi la polisi,  kutokana na idadi kubwa ya vifo na majeruhi wa ajali za barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini,  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara hasa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973,” aliongeza Sanga

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani kutokana na tafiti mbalimbali zilizokwisha fanyika wanakiri kwamba pale ambapo pamekuwa na sheria  madhubuti za usalama barabarani idadi ya ajali zinazozuilika imeweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Tanzania ni lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani ili kukomesha hali hii.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles