27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Tambwe bado mtamu, atupia mabao manne Championship

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba, Amissi Tambwe, imedhihirisha kuwa bado ni mkali katika  ufungaji baada ya leo,  Oktoba 2, kuifungia timu yake ya   DTB mabao  manne katika ushindi wa 4-1 dhidi ya  African Lyon.

Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Championship zamani Daraja la Kwanza, uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Tambwe alifunga mabao hayo dakika ya 12,40,46 na 54, huku la African Lyon likifungwa na  Twaha Mvuma.

Tambwe amejiunga na DTB msimu pamoja na wachezaji wengine nyota waliowahi kutamba Ligi Kuu Tanzania Bara kama vile Juma Abdul, David Mwantika, Yusuf Mlipili, Nicholas Gyan na James Msuva

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles