24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 20 washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim, amesema tukio hilo limetokea mnamo septemba 29 mwaka huu majira ya saa 11 jioni huko maeneo ya kitongoji cha Mgamba, Kijiji cha Dakawa , kata ya Bwakila chini, Wilaya na Mkoa wa Morogoro .

Kamanda Musilim amemtaja marehemu kuwa ni Juma Katinda (58), mkulima na mkazi wa dakawa, ambae aliuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi kisha mwili wake kuuteketeza kwa moto.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni kwamba, marehemu alichoma moto nyumba iliyojengwa na jirani yake aliyejulikana kwa jina moja la ruchamla karibu na eneo lake.

“Marehemu  alikuwa safarini na aliporudi nyumbani aliona ujenzi huo ndipo alipo chukua uamuzi wa kuichoma moto, kwa madai ya kwamba lile lilikuwa ni eneo lake” amesema Kamanda Musilim.

Aidha amesema baada ya marehemu kuchoma moto nyumba hiyo wananchi walijitokeza ili kutoa msaada, ila  alizuia watu wasitoe msaada ndipo wananchi wakaitana kwa wingi kisha kumzingila na kumshambulia kwa silaha za jadi hadi kumuua kisha mwili wake kuuteketeza kwa moto.

“Baada ya uchunguzi wa kina na msako mkali tumefanikiwa kukamata watuhumiwa 20 na tunaendelea na kuwahoji, ambapo 8 kati yao walikamatwa ndani ya  bus wakiwa katika harakati za kutoroko” ameeleza Musilim.

Hata hivyo kamanda musilim baada ya kuongea na wananchi wa bwakila chini, amewataka kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mikononi, na kisha kuwatembelea na kuwapa pole familia ya marehemu iliyo okolewa katika tukio hilo ambapo marehemu alikuwa na wake 03 , watoto, ndugu na jamaa jumla yao watu 11 ambao  wamepewa hifadhili katika kituo cha polisi Duthumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles