27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tamasha la Sanaa Bagamoyo latinga siku ya pili

WAKATI Tamasha la 34 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo likiwa limeanza jana kwa maandamano ya kuzunguka mitaa mbalimbali ya mji wa Bagamoyo, leo wadau mbalimbali wa sanaa wanapata mafunzo ya kupinga rushwa yanayoratibiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Katika warsha hiyo pia mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali, maofisa kutoka ofisi mbalimbali na wizara mbalimbali wamealikwa ili kupata mafunzo hayo yatakayosaidia kupinga na kukabiliana na rushwa hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.

Licha ya warsha hiyo juu ya rushwa kuendelea, Katibu wa Tamasha hilo, Benjamin Mahimbali, alisema warsha nyingine ikiwemo ya kupinga mauaji ya albino na haki za binadamu zitafanyika siku zijazo katika tamasha hilo.

Maandamano ya uzinduzi wa tamasha hilo yalifanyika juzi usiku saa nane hadi saa 9.30 yalipopokelewa na mgeni rasmi ambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo hicho, Rashid Masimbi na kuendelea na shughuli za uzinduzi katika viwanja vya chuo hicho hadi saa 11 jioni.

Onyesho kamili la uzinduzi lilianza saa 2 usiku kwa vikundi mbalimbali vya ngoma, maonyesho ya sarakasi na nyimbo mbalimbali kutumbuiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles