Upendo Mosha, Moshi
Killfair Promotion inakusudia kufanya tamasha kubwa la kimataifa lijulikanalo Kama Octoberfest lenye lengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo kinywaji cha bia.
Tamasha hilo ambalo linarajiwa kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya 2000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki litalofanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia tamasha hilo kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Killfair Promotion, Dominic Shoo amesema tamasha hilo litakuwa na fursa ya bidhaa za Tanzania ikiwemo bia katika ngazi mbalimbali za kimataifa.
“Tamasha hili litafanyika Octoba 11 na 12 Mjini Moshi na lengo letu ni kutangaza bidhaa za hapa nchi ikiwemo vyakula na vinywaji vinavyozalishwa hapa nchi naamini baada ya tamasha hili bidhaa za hapa nyumbani zitapata soko” amesema Shoo.