29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TAKWIMU UBAKAJI, ULAWITI WATOTO ZATISHA

Na AGATHA CHARLES


MATUKIO ya ukatili wa kijinsia kwa watoto yameonekana kuongezeka yakilinganishwa na mwaka jana, baada ya takwimu mpya kuonesha kuwa, tangu Januari hadi Juni, mwaka huu, watoto 2,365 walibakwa, huku 533 wakilawitiwa.

Takwimu hizo, ambazo gazeti hili limezikusanya kutoka ndani ya Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa, zimeonesha kuwa, pamoja na idadi hiyo kubwa ya watoto kubakwa, watoto wa kiume waliolawitiwa kati ya 533 walikuwa ni 463, huku wa kike wakiwa 70.

Kwa upande wa watoto walionajisiwa katika kipindi hicho cha Januari hadi Juni, wa kiume walikuwa ni wanane, huku wa kike wakiwa ni wanne.

Taarifa hiyo haikuweka wazi mikoa inayoongoza kwa mwaka huu kwa vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto.

Wakati takwimu za mwaka huu zikionesha hivyo, mwaka jana kuanzia Januari hadi Desemba zilionesha kuwa, watoto waliobakwa walikuwa 2,984.

Watoto wa kiume waliolawitiwa walikuwa 442, na 59 ni wasichana na walionajisiwa wakiwa ni wanne na msichana mmoja.

Kwa mwaka jana, idadi hiyo ilionekana kupungua ikilinganishwa na ile ya mwaka 2016, ambako watoto waliobakwa walikuwa 4,423, huku wavulana waliolawitiwa wakiwa 488 na wasichana 48.

Katika kipindi hicho cha mwaka jana, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilionesha kuwa, katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2017, jumla ya matukio 13,457 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto yaliripotiwa ikilinganishwa na matukio 10,551 kipindi kama hicho mwaka 2016.

Katika ripoti hiyo ya NBS ya mwaka jana, ilionesha kuwa, mikoa iliyoongoza ilikuwa ni Mjini Magharibi, ambayo watoto waliobakwa walikuwa 371, Tanga 223, Temeke 209, Kinondoni 163, Mbeya 147, Ilala 146, Dodoma 136, Rukwa 131 na Tabora 105.

Inaendelea……………… Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA JUMAMOSI

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles