25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BOSI TWAWEZA KIKAANGONI

Na ANDREW MSECHU


IKIWA ni takribani mwezi mmoja tangu Taasisi ya Twaweza ilipotoa ripoti za tafiti zilizofanya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuiandikia barua ijieleze kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa madai ya kuvunja sheria za tafiti, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo naye sasa anahojiwa na Idara ya Uhamiaji juu ya uraia wake.

Julai 5, Twaweza ilitoa ripoti mbili za sauti za wananchi zenye vichwa vya habari; ‘Kuwapasha Viongozi?’ na ‘Nahodha wa Meli yetu wenyewe’, ambazo pamoja na mambo mengine, zilionyesha umaarufu wa Rais, wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na vijiji na vyama vya siasa umeshuka.

Siku nne baada ya kutangazwa kwa matokeo ya ripoti hizo, COSTECH iliandikia Twaweza  barua Julai 9, ambayo ilisainiwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Dk. Amos Nungu.

Barua hiyo ilisema taasisi hiyo ilikiuka sehemu ya 11 ya Mwongozo wa Taifa wa Usajili na Utoaji wa Matokeo ya Tafiti, hivyo ijieleze kwanini isichukuliwe hatua.

Wakati umma ukisubiri kujua hatima ya COSTECH na Twaweza, jana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Aidan Eyakuze, alizungumza na waandishi wa habari na kusema hati yake ya kusafiria inashikiliwa na Uhamiaji.

Alisema Idara ya Uhamiaji imeishikilia pasi yake tangu Julai 24 na kwamba tangu pasi hiyo iliposhikiliwa hakupewa sababu.

Alisema Agosti mosi alizuiwa kusafiri kwa kutumia shahada ya dharura ya kusafiria iliyotolewa kwa utaratibu halali.

Alisema safari yake iliyozuiliwa ilikuwa ni ya Nairobi na Kampala, ambako alikuwa anakwenda kushiriki mikutano ya kikazi kwenye ofisi za Twaweza zilizo Kenya na Uganda.

“Hadi sasa hatuna taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hili,” alisema.

Uhamiaji

Kutokana na madai hayo ya Eyakuze, gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda, ambaye aliieleza Mtanzania Jumamosi kuwa, wameishikilia pasi ya kusafiria ya Eyakuze kwa sababu za kiuchunguzi.

Alisema wameishikilia baada ya kupata taarifa za utata wa uraia wake kutoka kwa raia wema, hivyo kama ilivyo majukumu ya Idara hiyo, walimwita na kuishikilia pasi hiyo kwa ajili ya uchunguzi.

“Huu kwetu ni utaratibu wa kawaida. Ni sehemu ya majukumu yetu ya kila siku. Kwa sasa tunaendelea na uchunguzi na ndio utakaobainisha kama ni raia au siyo raia, lakini nikwambie tu kwamba hili si suala jipya wala si la ajabu,” alisema Eyakuze.

Inaendelea…………. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles