24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yawafikisha viongozi 6 mahakamani

Abdallah Amiri, Igunga.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imewakamata viongozi sita wa Chama cha Msingi cha Wakulima wa zao la pamba (AMCOS) wa Kijiji cha Choma na kuwafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi Wilaya ya Igunga kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wakulima.

Waliofikishwa mahakamani mwishoni mwa wiki iliyopita, ni Mwenyekiti wa Baumu Amcos, Nyolobi Nangale (36), Sylivester Masanyigule(46), Andrew Senga(49), Iwize Masanja(37), Martine Silas(31), Elias Kelege(25) wote wakazi wa Kijiji cha Choma.

Mwendesha Mashtaka wa taasisi hiyo,Mazengo Joseph aliiambia mahakama mbele ya Hakimu Lydia Ilunda kuwa washtakiwa wote walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)(2) na 3(a) sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11 ya 2007.

Alisema washitakiwa wote,wanakabiliwa na mashtaka matatu.

Alisema shtaka la kwanza, kati ya Agosti mosi, mwaka huu na Oktoba 25, mwaka huu kwa muda tofauti katika Kijiji cha Choma, washtakiwa wote kwa pamoja waliomba rushwa ya  800,000 kutoka kwa Kulwa Mabula ili waweze kumlipa fedha zake za pamba Sh milioni 8,345,220 alizokuwa ameiuzia pamba Kampuni ya OLAM.

Shtaka la pili, linalowakabili washtakiwa wote katika tarehe hiyo na muda tofauti, waliomba rushwa ya Sh 600,000 kutoka kwa Shimbi Ganja ili waweze kumlipa fedha zake Sh  6,536,400 alizokuwa ameuza pamba kwenye kampuni ya OLAM.

Alisema shtaka la tatu, katika tarehe hiyo na muda tofauti waliomba ruhswa ya Sh 600,000 kutoka kwa Shimbi Kadengu ili waweze kumlipa fedha zake Sh milioni  6,220,680 aliyouza pamba kwa kampuni ya OLAM.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo waliyakana yote ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 6, mwaka huu itakapotajwa tena ambapo washitakiwa wawili wamedhaminiwa kwa dhamana ya Sh  milioni  5 kila mmoja, huku wanne wakipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles