28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Taifa Stars, Kenya zatoka sare

taifa starsNA MWANDISHI WETU,

TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi.

Mchezo huo ulikuwa wa maandalizi kwa timu zote, kwani zinajiandaa na mechi za makundi kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), ambapo Taifa Stars inatarajia kumenyana na Misri Juni 4, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa,  Dar es Salaam.

Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha, Charles Boniface Mkwasa, kiliingia uwanjani bila ya nyota wake wawili wanaocheza soka la kulipwa ambao ni Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu anayekipiga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Samatta alikua anaitumikia timu yake iliyokua inawania kufuzu kucheza Kombe la Europa wakati Ulimwengu aliumia lakini wote wanatarajiwa kutua nchini Juni 3, mwaka kuikabili Misri.

Mchezo wa jana ulianza kwa kasi ambapo timu zote zilishambuliana kwa zamu, huku safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars iliyoongozwa na Elius Maguli ikilisakama lango la Kenya.

Mashambulizi hayo yaliisadia Taifa Stars ambapo Maguli aliifungia bao la kuongoza dakika ya 32 baada ya kupokea krosi safi iliyopigwa na Juma Abdul.

Bao hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani Kenya walifanikiwa kusawazisha katika dakika ya 39 kupitia kwa kiungo wake, Victor Wanyama, aliyefunga kwa penalti baada ya mlinzi wa Taifa Stars, Abdul kucheza rafu mbaya Ayoub Timbe.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana katika kipindi cha pili kwa kila moja kusaka bao la ushindi, lakini hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika hakuna timu iliyifanikiwa kupata bao la ushindi.

Katika michuano ya AFCON, Taifa Stars inakabiliwa na kibarua kigumu katika Kundi G ikiwa inashika  nafasi ya mwisho kwa kujikusanyia pointi moja iliyopata dhidi ya Nigeria, baada ya kujitoa kwa Chad na kupokonywa pointi tatu za ushindi ilizozipata mjini N’Djamena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles