23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tafuteni suluhu ya soko kwa bidhaa za Tanzania-Dk. Mpango

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amezitaka Wizara za Bara na Zanzibar kushirikiana na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki kuweka nguvu zaidi katika kutanzua tatizo la masoko kwa bidhaa za Tanzania.

Pia amezitaka Taasisi za Utafiti kufanya utafiti za mbegu ili kujua ni mbegu gani kama tukiwekeza tunaweza kupata mafuta ya kutosheleza.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 13, 2022 wakati akifunga maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Dk. Mpango amesema upatikanaji wa vifungashio vyenye ubora umekuwa ni changamoto kwa wafanyabiashara wengi.

“Nimepata bahati ya kuwatembelea baadhi ya wafanyabiashara kilio chao kikubwa ni kuhusiana na vifungashio vyenye ubora lakini pia vifungashio hivyo vinauzwa kwa bei ya ghali sana”,alisema dkt mpango .

Alisisitiza kuwa wazalishaji wanapaswa kuzingatia kanuni za ushindani ili ziweze kuleta ushindani katika bidhaa wanazozizalisha. Ni vyema wafanyabiashara wakaendelea kuzalisha bidhaa zenye mahitaji makubwa kwa watanzania ili kuweza kujitegemea wenyewe,” amesema Dk. Mpango na kuongeza kuwa:

“Wengi tunakumbuka namna janga la ugonjwa wa Uviko-19 ulivyoathiri uchumi wa nchi lakini pia kwa wafanyabiashara wadogo hili liwe funzo kwetu sisi wafanyabiashara kwa kuweza kuwekeza kidigital ili itakapotokea ugonjwa wa mripuko kuweza kujiendesha kiuchumi,” amesema Dk. Mpango.

Amesema maonyesho ya mwaka huu yamekuwa ya kipekee kwani yameweza kuongeza idadi ya watu mara mbili ya maonyesho ya 45 .

Ameongeza kuwa wananchi na wafanyabiashara waendelee kutoa maoni ya namna ya kuboresha bidhaa ya maonyesho yanayokuja.

Pia amewataka wajasiriamali kuzitumia fursa za mafunzo zinazotolewa Kwa wafanyabiashara ili kuweza kuboresha biashara zao.

Awali, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashantu Kijaji alisema serikali itaendelea kusimamia sheria na kanuni mbalimbali ili ziendane na mazingira ya sasa.

“Tunakwenda kukaa pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali ili kuweza kuzalisha bidhaa za mafuta ambapo tunaona soko letu la dunia limetikisika,” amesema Waziri Kijaji.

Hata hivyo, alisema kupitia kliniki ya biashara iliyokuwepo katika maonesho hayo wadau 93 wamehudumiwa, changamoto 120 zimeshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa papo hapo na 83 ziliwataka kugusa sheria mbalimbali.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Khamis amesema katika maonesho hayo kumekuwa na ongezeko la waliotembelea kutoka 227,815 mwaka jana hadi kufikia 315,000.

“Tutaendelea kusimamia vyema taasisi yetu pamoja na kuboresha maonesho haya ili yawe na tija zaidi kwa miaka ijayo,” amesema Latifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema wataendelea kuhakikisha Dar es Salaam kama mji wa biashara unaendelea kupendeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles